WIZKID APANIA KUFANYA MAKUBWA 2017 ZAIDI YA MWAKA JANA

MKALI wa muziki nchini Nigeria, Ayodeji Ibrahinm “Wizkid” amedai anatarajia kufanya makubwa mwaka huu na hana mpango wa kuangalia aliyoyafanya mwaka jana.  

Msanii huyo mwenye umri wa miaka 26, alifanya makubwa kwa kufanya kazi na nyota wakubwa wa muziki duniani akiwemo Drake na Chris Brown.

“Mwaka jana nilifanya makubwa pamoja na kununua nyumba nchini Marekani, lakini mafanikio hayo si kitu chochote kwangu, natarajia kufanya makubwa zaidi mwaka huu.”


“Kwa sasa nipo katika mapumziki hadi Februari, mwaka huu. Sina mpango wa kuangalia nilikotoka, nataka niwe kama nimezaliwa upya huku nikiwa na kiu ya mafanikio,” aliandika Wizkid.

No comments