YAH TMK WATUA BULYAGA... sasa kupatikana hapo kila Jumatano kuanzia kesho

YAH TMK Jumatano zote kuanzia kesho watakuwa wanapatikana ndani ya Bulyaga Temeke, jijini Dar es Salaam kwa kiingilio cha buku tano tu.

Meneja wa bendi hiyo iliyo chini ya bosi wa kituo cha Mkubwa na Wanawe, Said Fella, Muddy K ameiambia Saluti5 kuwa shoo hiyo inatokana na maombi mengi na ya muda mrefu ya mashabiki wao wa eneo hilo.

“Tutakuwa tukipatikana bulyaga kuanzia sasa, kwahiyo wakazi wa Temeke nafikiri kuanzia sasa watakuwa wamepata sehemu ya kufurahia “middle weekend” yao kila wiki,” amesema Muddy K.

Meneja huyo amesema kuwa shoo hiyo itakuwa pia ikinogeshwa na surprise mbalimbali za kila wiki pamoja na zawadi kemkemu kwa mashabiki wao watakaokuwa wanahudhuria mara kwa mara.

No comments