Habari

YEMI ALADE AALIKWA TUZO ZA GRAMMY… afurahia na kusema ni tuzo ya mashabiki wake

on

NYOTA wa muziki nchini Nigeria,
Yemi Alade ametumiwa mwaliko wa kuhudhuria tamasha la utoaji tuzo za Annual
Grammy Awards ambazo zitatolewa Februari 12, mwaka huu.
Tuzo hizo za 99 zitatolewa
kwenye ukumbi wa Staples Center, Los Angeles, Marekani ikiwa ni mara ya kwanza
kwa msanii huyo kuhudhuria tamasha hilo kubwa.
Hata hivyo kupitia akaunti yake
ya Instagram, msanii huyo aliweka wazi mwaliko huo na kuwashukuru wote ambao
walimuunga mkono kwa mwaka 2016.

“Naamini nafasi hii nimeipata
kutokana na kujituma kwangu mwaka 2016 pamoja na mashabiki wangu kuonyesha
kunijali, ninawashukuru wote kwa kunijali na kuupenda muziki wangu,” alisema
Yemi.

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *