YOUNG DEE AGOMA KUUVUSHA MUZIKI WAKE NJE YA MIPAKA HADI KIELEWEKE BONGO

RAPA Young Dee amesema kuwa bado muziki wake haujapenya vizuri ndani ya nchi na kwamba hali hiyo inakwamisha mipango yake ya kujitangaza kimataifa kama wafanyavyo baadhi ya wasanii.

Alisema kuwa ataendelea kuelekeza nguvu zake kwenye soko la ndani hadi hapo atakapoona kwamba muziki wake umewafikia Watanzania wengi ndipo atakapoanza harakati za kusaka soko la kimataifa.


“Ninachoamini ni kwamba msanii hawezi kufanya vizuri kimataifa ikiwa nyumbani bado hafanyi poa, ndio maana ninasema kwamba siwezi kukimbiklia huko kabla ya kupata soko huku,” alisema Young Dee.

No comments