ZIMBABWE WAPANIA KUSHANGAZA FAINALI ZA KOMBE LA MATAIFA AFRIKA

ZIMBABWE imepania kushangaza kwenye michuano ya fainali Kombe la Mataifa Afrika zitakazofanyika Januari 14 nchini Gabon.

Nchi hiyo inawategemea zaidi wakali wake Knowledge Musona anayesakata soka nchini Ubelgiji na mkali wa Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini, Khama Billiat.

Pamoja na matatizo ya kiuchumi yanayoikabili nchi hiyo lakini bado imepania kupigana kufanya vizuri katika mashindano hayo.


Hata hivyo, inakabiriwa na mtihani mgumu wa kuzikabili Algeria, Senegal na Tunisia katika Kundi B.

No comments