ZINEDINE ZIDANE APANGA KUMPUMZISHA CRISTIANO RONALDO

KOCHA wa Real Madrid, Zinedine Zidane amepanga kumpumzisha nyota wake tegemeo, Cristriano Ronaldo.

Zidane alisema wamekubaliana na nyota huyo apumzike baadhi ya mechi ili awe fiti kuiongoza timu hiyo kufanya vizuri katika mashindano mbalimbali msimu huu.

“Nimezungumza na Ronaldo juu ya umuhimu wa kupumzika baadhi ya mechi na amekubali ushauri wangu,” alisema Zidane.


Ronaldo alikosa mechi ya Kombe la Copa del Rey dhidi ya Siville Jumatano iliyopita.

No comments