ALLY CHOCKY NA CHAZ BABA WAKO BARIADI LEO USIKU …ni katika ile ‘tour’ ya miaka 30 kwenye ‘game’


Mwimbaji nyota wa Twanga Pepeta Ally Chocky, leo atakuwa Bariadi ambapo usiku ataangusha show ya Valentine’s Day.

Chocky atakuwa sambamba na nyota wa zamani wa Twanga Pepeta Chaz Baba kwenye onyesho hilo litakalofanyika katika ukumbi wa CK Club.

Onyesho hilo ni sehemu ya ziara ya Chocky ya kusherehekea miaka yake 30 kwenye ‘game’ ya muziki wa dansi.

Ziara hiyo ya Chocky itaendelea siku ya Ijumaa ambapo atatumbiza Tarime katika ukumbi wa PKM huku Jumamosi hii itakuwa zamu ya Musoma mjini ndani ya ukumbi wa Dream Garden.

No comments