Habari

ANTOINE GRIEZMANN AINGIA RADA ZA BAYERN MUNICH

on

KLABU ya Bayern Munich imemweka katika orodha ya usajili ujao Antoine
Griezmann.
Lengo la kufanya hivyo ni mkakati wa vigogo hao wa Bundesliga wanaotaka
kuwa na kikosi kipana cha kupambana kwa ajili ya kusaka mataji zaidi.
Katika kuhakikisha hilo linafanikiwa, Bayern wameanzisha ushawishi kwa
uongozi wa klabu yake ya sasa ya Atletico Madrid ili wakubali kuweka mezani
kitita cha usajili ujao wa majira ya baridi mwezi Januari na ule wa kiangazi.
Griezmann mwenye umri wa miaka 25, alikuwa katika kiwango bora katika
michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya na huku akionyesha kiwango kizuri ndani ya
Atletico Madrid.
“Tunapambana kuona Griezmann anatua Bayern, ni mchezaji wa aina yake ambaye
atakuwa na msaada ndani ya kikosi,” imekiri klabu ya Bayern Munich katika
tovuti yao.

Hata hivyo, Bayern wataingia katika upinzani wa baadhi ya timu zinazomwania
nyota huyo, kwani Chelsea na Barcelona nazo zinapiga hesabu kali za kupata
saini yake.

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *