Habari

ANTONIO CONTE ATULIZA PRESHA YA CESC FABREGAS CHELSEA

on

KUNA kauli
ambayo kocha wa Chelsea alimwambia Cesc Fabregas inayoonyesha kumshusha presha
kiungo huyo.
Unajua amemwambiaje?
Antonio Conte amemwambia kiungo huyo raia wa Hispania kuwa asikate tamaa ya
kubakia Stanford Bridge kwani amemweka katika orodha ya wachezaji muhimu kikosini.
Lakini Conte
amemweleza fabregas kuwa pamoja na kauli hiyo, lazima akaze buti kwani
ushindani ni mkubwa ndani ya msimu huu.
Kauli ya
kocha wa matajiri hiyo inakuja siku chache ambapo kiungo huyo amekuwa akipangwa
katika mechi nyingi muhimu.
“Cesc yumo
katika mipango yangu ya kuimarisha kikosi cha msimu huu.”
“Ninachoshukuru
ni kwamba ni mmoja ya wachezaji walio na uzoefu mkubwa wa Ligi, msaada mkubwa.”

“Ninampa
nafasi katika mechi kadhaa za kuibeba timu na ninaamini ana uwezo wa kuonyesha
kiwango chake cha misimu miwili iliyopita,” alisisitiza Conte.

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *