ARSENE WENGER ATAKA LUCAS PEREZ APEWE MUDA KUONYESHA CHECHE ZAKE

KOCHA wa Arsenal, Arsene Wenger amekiri kwa kusema kuwa nyota wake Lucas Perez amebidsha hodi na hivyo anatakiwa kutoa muda ili aweze kuonyesha makali yake.

Awali Mhispania huyo alikuwa akitajwa kuwa ataondoka ifikapo mwishoni mwa msimu huu baada ya kukosa nafasi ya kucheza mara kwa mara chini ya Wenger.

Hata hivyo juzi alivyopewa nafasi ya kucheza Perez ndiye aliyefunga bao la kwamba katika ushindi wao wa 2-0 dhidi ya Sutton United katika mchezo wa Kombe la FA.

Kutokana na kiwango alichokionyesha nyota huyo Wenger anasema kuwa straika huyo wa zamani wa timu ya Deportivo La Coruna ambaye msimu huu amecheza kwenye kikosi cha kwanza mara mbili anatakiwa kupewa muda.

“Ndio, ni kama kabisha hodi lakini nina mastaraika wengi,” alisema Wenger.


“Nina Olivier Giroud, Danny Welbeck, Theo Welcott, Alexis Sanchez na Lucas lakini ni kweli anatakiwa kutumika kwa sababu amefunga bao na ni mchezaji mzuri,” aliongeza juzi Mfaransa huyo.

No comments