AUNTY EZEKIEL: BONGOMUVI TUNAIUA WENYEWE BAADHI YA WASANII

KIMWANA mwigizaji wa filamu nchini, Aunty Ezekiel amewarushia lawama wasanii wenzake kuhusu kushuka kwa Bongomuvi akidai kuwa baadhi yao wamechangia kuwepo kwa hali hiyo.

Msanii huyo alisema kuwa mtindo wa kujihusisha na matendo machafu ni chanzo cha kushuka kwa soko la filamu nchini ingawa kumekuwa na visingizio vingi ambavyo havihusiani na hilo.

“Suala la kushuka kwa soko la filamu nchini limechangiwa na wasanii wenyewe kwani wapo baadhi ambao wamekuwa wakishiriki mambo machafu kama njia ya kutafuta kiki za kuwapandisha na kumbe wanaharibu fani,” alisema.

Alisema kuwa umefika wakati sasa wasanii wabadilike kuanzia wenye majina makubwa na hata wanaochipukia kwa kuandaa kazi zenye ubora zitakazowatangaza badala ya kuendeleza skendo wakidhani zitawasaidia.

No comments