BAADA YA KUTIMUA KOCHA LEICESTER CITY YAFUFUKIA KWA LIVERPOOL KWA USHINDI WA 3-1


Leicester City imeonyesha maajabu baada ya kuinyuka Liverpool 3-1 kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya England.

Ikicheza mchezo wake wa kwanza bila kocha Claudio Ranieri aliyetimuliwa, ikawachukua Leicester dakika 28 kupata bao la kuongoza kupitia kwa mshambuliaji wao hatari Jamie Vardy, kabla Danny Drinkwater hajatupia la pili dakika ya 39.

Dakika ya 60 Jamie Vardy akarejea tena kwenye kitabu cha magoli kwa kufunga bao la tatu huku
Philippe Coutinho akiifungia Liverpool goli la kufutia machozi dakika ya 68.

Kwa matokeo hayo, Liverpool inaendelea kubaki nafasi ya tano ikiwa na pointi 49 kwa michezo 26 na kuruhusu kupumuliwa kwa kasi na Manchester United yenye pointi 48 na mchezo mmoja wa kiporo mkononi.

No comments