BAO LA UTATA LA BARCELONA LALAZIMISHA TEKNOLOJIA YA VIDEO HISPANIA

KUFUATIA utata wa bao la Barcelona lililokataliwa wikiendi iliyopita kwenye mechi ya Ligi Kuu Hispania dhidi ya Real Bets, sasa mipango inafanyika ili teknolojia ya video itumike kusaidia kuamua soka huko.

Mwamuzi wa mchezo huo alikataa bao kufuatia shuti la Jordi Alba ambalo liliokolewa na mchezaji wa Real Bets wakati mpira ukiwa umevuka mstari wa goli.

Picha za marudio ya televisheni zilizoonyesha dhahiri kuwa mpira huo ulikuwa umevuka mstari.

Rais wa Ligi Kuu Hispania, Javier Tebas alisema wako tayari kutumia teknolojia ya video kuanzia mwakani lakini baada ya kupitishwa na Shirikisho la soka la kimataifa (FIFA).


Kufuatia tukio hilo la mechi ya Barcelona, wadau wengi wa soka nchini Hispania wamelilia kuanzishwa kwa matumizi ya teknolojia ili kukabiliana na uamuzi wenye utata.

No comments