Habari

BAYERN MUNICH WAGOMA KUFANYA USAJILI WA KISHINDO

on

KIGOGO wa
Bundesliga na mabingwa watetezi wa Ujerumani, Bayern Munich wamesema hawana
haja ya kufanya usajili wa kutisha kutokana na ukweli kuwa kikosi chao kipo
kamili na kimetimia.
Mkurugenzi wa
michezo wa klabu hiyo kongwe alithibitisha taarifa za kutosajili katika usajili
wa majira ya kiangazi.
“Hatuna
tulichokipanga kuhusu usajili mpaka sasa. Ni sawa na kusema, hatuna haja ya
kufanya hivyo labda itokee lolote la dharura,” alisema Sammer.
“Tuna
wachezaji wachache wa kuwarejesha kikosini Holger Badstuber amerudi na David
Alaba pia amerudi katika kiwango chake.”
“Tumemuuliza
kocha wetu kuhusiana na suala la kusajili akatuhakikishia kuwa hakuna haja ya
kufanya usajili mkubwa akiamini kuwa kikosi kipo imara kwa ajili ya msimu huu.”

“Ila tumempa
fursa ya kuangalia kama anaweza kufanya usajili katika muda mwafaka, nae
amejibu kuwa ataangalia kama kuna haja ya kuongeza wawili ama watatu, ila
amejiridhisha kuwa na kikosi bora cha kutetea ubingwa kwa mara nyingine msimu
huu,” alisema Mkurugenzi huyo.

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *