BEKI KURT ZOUMA AAMINI CONTE ATAMREJESHA KIKOSI CHA TIMU YA TAIFA UFARANSA

BEKI ambaye amerejea kwenye makali katika kikosi cha Chelsea, Kurt Zouma amesema kwamba chini ya kocha wake wa sasa, Antonuio Conte atazidi kuwa mkali zaidi.

Nyota huyo raia wa Ufaransa amesema kwamba wakati anaendelea kuuguza goti alikuwa hana uhakika wa kurejea katika kikosi cha kwanza lakini sasa anamshukuru Mungu kwa sababu yuko katika makali mapya.

Kurt Zouma amekiri kwamba kulikuwa na wasiwasi na tayari alishaanza mazungumzo na Chelsea kuhusu uwezekano wa kuachana na klabu hiyo, lakini sasa anafurahi kuona yuko kwamba yuko katika kiwango bora.

“Maumivu yalikuwa makali sana na kila mmoja alikuwa anajua kwamba mwisho wangu wa kucheza klabu hii ni kama umefika, lakini sasa ninachowaza ni kingine kabisa,” amesema.

Nyota huyo amesema kwa sasa anajua kwamba kama akiendelea kuaminiwa na kocha Antonio Conte anaweza pia kurejea kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Ufaransa.

Kwangu mimi kama mchezaji, naweza kurejea kwenye ubora wangu lakini ndoto yangu kubwa ni kucheza tena timu ya taifa. Kwa mipango yangu na jitihada za mwalimu najua inawezekana kabisa,” amesema.

Mchezaji huyo ameliambia jarida la L’Equipe hana wasiwasi kwamba Chelsea ndio itakuwa bingwa wa Ligi Kuu England na anajua kwamba maisha ya baadae yanayomuhusu yeye ni kufanya kazi na timu ya taifa zaidi.


“Hata wakati nilipokuwa mdogo nilikuwa na ndoto zangu. Lakini ndoto kubwa kwa kila mchezaji ni kucheza timu ya taifa kwa kiwango kikubwa,” alisema.

No comments