Habari

BENFICA YAKANUSHA KUMPIGA BEI VICTOR LINDERLOF

on

KLABU ya Benifica ya Ureno imekanusha tetesi za kumuuza mlinzi kijana
Victor Linderlof mwenye umri wa miaka 21.
Hatua ya klabu hiyo kukanusha inafuatia taarifa za kwamba timu kubwa za
barani Ulaya zimeingia vitani kwa ajili ya kusaka saini yake.
Timu mahasimu katika La Liga, Real Madrid na Barcelona ni kati ya vigogo
wanaotaka kumsajili wakati wa kipindi cha usajili cha dirisha la Januari
mwakani.
Pamoja na vigogo hao vya Ligi ya Hispania pia Manchester United wanatajwa
katika mbio hizo za kumwania nyota huyo wa klabu ya Benfica.
Mlinzi huyo kijana amekuwa katika kiwango bora katika msimu huu kiasi cha
kuzigonganisha timu kubwa kupata saini yake.
Imebainika kuwa Benfica imesitisha nia ya kumweka sokoni beki huyo baada
ya kuondokewa na mlinzi wao mahiri Renato Sanches aliyejiungana
Bayern.

Katika kuhakikisha Haimpotezi Lindelof, imeamua kuweka mezani ofa kubwa ya
euro mil 40 ambapo imebainika klabu ya Barca na Madrid wanaweza wasipande dau
hilo.

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *