BILL NAS AZIMA TETESI ZA KUTOELEWANA NA GODZILLA

RAPA Bill Nas amezizima tetesi zote za bifu baina yake na mkali Godzilla baada ya kuweka wazi kuwa hajawahi kugombana nae na kwamba hana tatizo lolote na mkali huyo anayetamba na ngoma ya “Kila Wakati”.

Bill Nas aliyasema hayo alipokuwa akihojiwa na kipindi cha “The Playlist” kinachoongozwa na mkali Lil Ommy kupitia Times Fm.


“Mimi na Godzilla tuko poa tu na mara ya mwisho alinipigia simu nikiwa Arusha na niliahidi kumtafuta ndani ya wiki hii sema nilikuwa bize na mitihani so nimemaliza juzi tu nadhani nitaonana nae ila sina shida yoyote na Godzilla,” alisema Bill Nas.

No comments