BURKINA FASO YAJIVUNIA NUSU FAINALI MATAIFA YA AFRIKA 2017

MSHAMBULIAJI mahiri wa Burkina Faso, Aristide Bance amesema timu yao imeweka heshima kufika hatua ya nusu fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika 2017.

Mchezaji huyo aliyefunga bao lililoipeleka Burkina faso nusu fainali ikiing’oa Tunisia, amesema kwamba ingawa Misri ni timu ngumu lakini nia yao ni kuitoa na kucheza fainali.

“Ingawa tumeifunga Tunisia, nadhani hata Misri tuna uwezo wa kuitoa, lakini itategemea na namna tutakavyojituma na kulinda lango letu. Vyovyote itakavyokuwa tunajivunia sana kufikia hatua hii, lengo letu lilikuwa ni kufika hatua ya mtoano,” alibainisha.


Mzaliwa huyo wa Ivory Coast aliyehamia mjini Ouagadougou akiwa na wazazi wake mwaka 2002 kwa sababu ya kukimbia vita, amesema ushindi wao ni zaidi kwa wananchi wote wa Burkina Faso.

No comments