CAF YAIPINGA GHANA MADAI YA VIWANJA VIBOVU KUWAJERUHI WACHEZAJI WAO

SHIRIKISHO la soka Afrika (CAF), limepinga madai ya Ghana kuwa wachezaji wake wamejeruhiwa kwa sababu ya viwanja vibovu vinavyotumika kwenye fainali za kombe la Mataifa Afrika (AFCON).

Kocha wa Ghana, Avram Grant alikaririwa mapema akidai wachezaji wake watano wameumia kutokana na ubovu wa viwanja vya Gabon.

“Hakuna ushahidi wa kisayansi unaothibitisha kuwa wachezaji wameumia kutokana na ubovu wa viwanja,” alisema msemaji wa CAF, Junior Binyam.

Uwanja ulioko mji wa Port-Gentil ndio umelalamikiwa zaidi kutokana na kuwa mbovu.


Binyam alijitetea kuwa suala la wachezaji kuumia sio la ajabu na kutolea mfano hata kwenye Ligi Kuu England wachezaji wengi tu wamekuwa wakiumia.

No comments