CAMEROON MABINGWA WAPYA AFCON, MISRI YALALA 2-1


Cameroon imetwaa ubingwa wa Kombe la Mataifa ya Africa (AFCON) baada ya kuilaza Misri 2-1 kwenye mchezo mkali wa fainali.

Misri ilikuwa ya kwanza kupata bao kupitia kwa kiungo wa Arsenal, Mohamed Elneny aliyefunga katika mazingira magumu kunako dakika ya 22, bao lillodumu hadi mapumziko.

Dakika ya 59 Cameroon wakasawazisha kwa kichwa kilichopigwa na beki Nicolas N'Koulou kabla Vincent Aboubakar hajatupia la ushindi dakika ya 88.

Cameroon sasa wanashika nafasi ya pili kwa kutwaa taji hilo mara nyingi (mara tano) wakiwa nyuma ya Misri iliyonyakua ubingwa mara nane.

No comments