CHELSEA, MANCHESTER CITY ZAJIPANGA KUPAMBANA KUMWANIA ISCO

TIMU za Chelsea na Manchester City zinaripotiwa kujipanga kuingia katika vita ya kumwania kiungo wa Real Madrid, Isco pindi dirisha wa majira ya joto litakapofunguliwa.

Kwa mujibu wa gazeti la Marca, vita hiyo imeibuka baada ya staa huyo wa timu ya taifa ya Hispania kuamua kuitema klabu hiyo ya Santiago Bernabeu ifikapo wakati huo na ni kwamba ni mmoja wa wachezaji ambao wameshafanya mazungumzo na Chelsea.


Hata hivyo, pamoja na kuwepo na mazungumzo hayo, kuna tetesi kuwa kocha wa Man City, Pep Guardiola ana uhakika nyota huyo anatamani kujiunga nae kwenye klabu hiyo ya Etihad Stadium huku pia Juventus nao wakitajwa kumtamani Mhispania huyo.

No comments