CHELSEA YAHAHA KUSAWAZISHA TAARIFA ZAKE DHIDI YA DAVID LUIZ

HIVI sasa klabu ya Chelsea inahangaika kujisafisha kutokana na taarifa yake kukinzana na mlinzi wake David Luiz raia wa Brazil.


Mchezaji huyo aliumia goti na klabu ikatoa taarifa haraka kuwa yuko fiti lakini baadae Luiz akatupia picha kwenye mtandao wa kijamii ikimuonyesha amevishwa mavazi maalum ya chumba cha upasuaji huku akiwa na kifaa maalum cha usoni.

No comments