CHIPUKIZI WA KIKE WA FILAMU PAKISTANI AILILIA NYOTA YA SHAH RUKH KHAN

MWIGIZAJI kinda wa kike wa Pakistani, Mahira Khan amesema pamoja na kujitosa kwenye filamu za Bollywood, kiu yake kubwa ni kufunika.

Alisema kwa sasa hakuna mpenzi wa filamu asiyeijua kazi iitwayo “Raees” iliyochezwa na nyota anayekubalika zaidi nchini Pakistani, Shah Rukh Khan ambaye pia anatamba kwa sasa ndani ya Bollywood.

“Kwa hakika ndoto zangu ni kuona kuwa siku moja ninakuwa staa kama alivyo Khan, ukienda kila pembe ya Pakistan huwezi kuona mcheza filamu anapendwa kama yeye,” alisema.


Hivi sasa Mahira yuko mbioni kutoa kazi yake mpya ambayo imeandaliwa na Rahul Dholakia na anasema itakapotoka lazima watu waipiganie.

No comments