CHUCHU HANS AWASHUSHUA WANAOTAKA WAACHANA NA RAY KIGOSI

NYOTA wa Bongomuvi, Chuchu Hans amesema kuwa watu waliokuwa wakitamani uhusiano wake na Ray uvunjike walie tu kwa madai kwamba mtoto wao amezidi kukoleza mapenzi yao.

Hivi karibuni msanii huyo alijifungua mtoto wa kiume aliyepewa jina la Jayden na Chuchu alisema kwamba mtoto huyo ni faraja kubwa katika uhusiano wao ambao baadhi ya watu wamekuwa wakiukodolea macho.

“Mapenzi yetu yamepitia changamoto nyingi na hasa baada ya baadhi ya watu kutamani tutengane lakini naamini wameshindwa kwa sababu mtoto amekoleza mapenzi yetu,” alisema Chuchu.


Chuchu alisema kuwa kilichobaki sasa ni kuendeleza mipango mingine zaidi ya kuimarisha uhusiano wao ikiwemo kufunga ndoa kwa vile anaamini waliokuwa wakiwaonea wivu wameshindwa.  

No comments