CRISTIANO RONALDO AENDELEA KUMBURUZA LIONEL MESSI

CRISTIANO Ronaldo amempiga bao tena hasimu wake, Lionel Messi.

Baada ya kushinda tuzo za Mwanasoka Bora Ulaya na FIFA, sasa inasemekana kuwa ndie mwanasoka aliyevuna fedha nyingi zaidi kwa mwaka 2016.

Ronaldo na Messi ambao ni wanasoka mahiri wanaotamba duniani, wamekuwa na ushindani mkubwa ndani na nje ya uwanja.


Kwa mujibu wa jarida la Forbes, Ronaldo alitengeneza kiasi cha pauni mil 70.6 kutokana na mshahara, bonas na shughuli za matangazo.

No comments