DAR MODERN KUTAMBULISHA TANO MPYA LEO USIKU KATIKA WA JAMVI LA JIJI


Kundi maarufu la muziki wa mwambao, Dar Modern Taarab, leo usiku litatambulisha nyimbo tano mpya katika show yao ya kila Ijumaa inayofahamika zaidi kama ‘Usiku wa Jamvi la Jiji’.

Nyimbo hizo zitatambulishwa katika ukumbi wao wa nyumbani ambao nao unaitwa Dar Modern, ulioko Magomeni Mikumi jijini Dar es Salaam.

Msemaji wa Dar Modern, Adam Mlamali ameiambia Saluti5 kuwa nyimbo hizo ni “Jaribosi”, “Kipi Chakula Kitamu”, “Nambie Nisichelee”, “Una Deni Lisilolipika” na “Paka Hakubali Kulala Chali”.

No comments