DAVID DE GEA ASHIKWA NA KIGUGUMIZI KUAMUA HATMA YAKE NDANI YA MAN UNITED

MLINDA mlango wa Manchester United, David de Gea amesema bado hajaamua mustakabali wa kandarasi yake ndani ya Old Trafford.

Hatua hiyo inafuatia swali aliloulizwa juu ya hatma yake pindi mkataba wake wa sasa ukifikia tamati huku akihusishwa pia kutakiwa na ama Real Madrid au Atletico Madrid.

Akihojiwa, De Gea alisema: “Ni mapema kusema nini kitatokea baadae kwani bado kuna mambo mengi ya kufanya nikiwa na United.”

“Kuna mazungumzo yanaendelea nikiwa hapa, naamini kila jambo litakwenda vyema, lakini nini kitaendelea ni jambo la kusubiri.”

“Nitazungumza kila jambo kwa wakati mwafaka, ingawa sitaki kuhusishwa na mimi kurejea Real Madrid, hapana.”


“Hiki ni kipindi ambacho kila siku kutakuwa na tetesi za usajili, lakini ukweli wa kila hatua utabakia katika suala la kusubiri hatma yangu ya baadae.”

No comments