DAWA ZA KUSISIMUA MISULI ZAMVUA TAJI BINGWA WA OLIMPIKI MEDALI YA DHAHABU URUSI

MWANARIADHA aliyeutwaa ubingwa wa Olimpiki na kuvishwa medali ya dhahabu katika mashindano ya Olimpiki London 2012, Mariya Savinova wa Urusi, amevuliwa taji lake.

Mshindi huyo wa mbio za mita 800 katika mashindano hayo ya London 2012, mbali ya kuvuliwa taji pia amepigwa marufuku kushiriki mashindano yoyote ya mbio hadi mwaka 2019.

Aidha, matokeo yote ya mbio za mwanariadha huyo tangu Julai 10, 2010 hadi Agosti 2013 yamefutwa baada ya kubainika kuwa alitumia dawa za kuongeza nguvu.


Taarifa kutoka katika mahakama inayosikiliza kesi ya makosa ya kimichezoimesema Savinona ni miongoni mwa wanariadha watano wa Urusi waliotajwa katika ripoti na mamlaka kuu ya kukabiliana na dawa za kusisimua misuli miongoni mwa wanariadha (WADA).

No comments