DAYNA NYANGE ATAMANI KOLABO NA WIZKID, PATORANKING

DAYNA Nyange amewataja mastaa wa Afrika ambao anatamani kufanya nao kazi.

Mkali huyo wa wimbo “Komela” amemtaja Wizkid na Patoranking, wote kutoka Nigeria, kuwa ndio wasanii anaowapenda na kuwafuatilia, hivyo anatamani kufanya nao kazi japo wapo wasanii wengine anaotamani kufanya nao.

“Nampenda Wizkid, ni mtu ambaye ninamuangalia kazi zake, Patoranking pia napenda kazi zake japo wapo wengi ambao natamani kufanya nao kazi,” Dayna amesema.


Wakati huohuo, Dayna ambaye hajawahi kufanya kolabo na msanii mwingine wa kike ameongeza kuwa kuna muda anafikiria kufanya nao kazi lakini pia inategemea na wazo la wimbo wake, japo ameahidi kufanya hivyo.

No comments