DEGO COSTA AVIPA MAKAVU VYOMBO VYA HABARI “VILIVYOMUHARIBIA”

MSHAMBULIAJI wa Chelsea, Diego Costa amevizodoa vyombo vya habari vilivyoripoti kuwa anakamilisha mipango ya kwenda kucheza soka China.

Mtangazaji wa radio wa Hispania, manu Carreno alidai hivi karibuni katika kipindi chake cha radio kuwa Costa ataondoka mwisho wa msimu huu kwenda China.

“Watu wanaongea ujinga mwingi kwenye vyombo vya habari, “Come one Chelsea” (Njooni Chelsea),” aliandika Costa kwenye akaunti yake ya Instagram.

Costa hivi karibuni aliwekwa benchi na kocha wa Chelsea, Antonio Conte baada ya kutokea mzozo baina yao kiasi cha kuwekwa benchi kwenye mechi na Leicester City na kutakiwa kufanya mazoezi yap eke yake.


Mshambuliaji huyo alijifanya ameumia lakini taarifa zinasema kuwa alikuwa amechanganywa na ofa ya dau kubwa kutoka China.

No comments