EDEN HAZARD ACHEKELEA MAISHA NA KIWANGO CHAKE BORA NDANI YA CHELSEA

STRAIKA Eden Hazard amesema kwamba kwa sasa anayafurahia maisha akiwa na klabu yake ya Chelsea baada ya kupambana na kisha akarejea katika kiwango chake.

Hazard alikuwa miongoni mwa wachezaji muhimu wakati  Blues walipotwaa ubingwa wa Ligi Kuu England msimu wa 2014/15 akiwa chini ya Jose Mourinho lakini msimu uliopita yeye na wenzake wakapoteza kiwango hivyo kuwafanya washindwe kutetea taji hilo.

Hata hivyo msimu huu vijana hao wa klabu hiyo magharibi mwa jiji la London wanaonekana kuimarika tangu alipowasili kocha wa zamani wa Juventus na timu ya taifa ya Italia Antonio Conte ambapo hadi sasa wapo mbele kwa pointi nane dhidi ya mahasimu wao katika msimamo wa Ligi hiyo.

Inaelezwa kuwa mchango wa nyota huyo wa timu ya taifa ya Ubelgiji ndiyo sababu ya kikosi hicho kuwa mbele katika msimamo huo.

“Msimu uluopita kila mtu alifahamu sikuwa katika ubora,” alisema Mbelgiji huyo.


Alisema kuwa kutokana na hali hiyo ndio maana msimu huu alisihama vyema akiwa hana majeraha jambo ambalo linamfanya kuwa tayari kucheza muda wote anapotakiwa.

No comments