FAINALI YA MISRI NA CAMEROON YAKUMBUSHIA MTANANGE WA MWAKA 2008

MCHEZO wa fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika mwaka 2017 ulipigwa jana Jumapili kati ya Misri ambao ni mabingwa mara saba wa AFCON na mabingwa mara tano, Cameroon.

Hata hivyo, mchezo huo ulikuwa ukikumbushia mchezo wa fainali za michuano hiyo mwaka 2008 walipokutana miamba hao.

Misri walitinga fainali wakilisaka taji lao la nane la michuano hiyo kwa mbinde kwani waliwatoa vijana wa Burkina Faso kwa mikwaju ya penati 4-3 baada ya timu hizo kumaliza dakika 90 bila kumpata mshindi na hata dakika za nyongeza hazikumpata mshindi.

Mwaka 2008 wakati Misri wakichukua Kombe lao la sita pale Accra, Ghana, waliwalaza Cameroon katika mchezo wa fainali.

Aidha mwaka 2010 nchini Angola, Misri walipochukua Kombe lao la saba, walicheza dhidi ya Ghana na kuibuka na ushindi usiotarajiwa na kuonekana kulitawala soka la Afrika.


Cameroon waliingia katika nusu fainali baada ya kuitoa moja ya timu bora katika mashindano haya, Senegal kabla ya kuwabanjua Ghana kwa mabao 2-0 katika nusu fainali.

No comments