Fernandinho amefichua kuwa alimshawishi Gabriel Jesus kukataa ofa za Barcelona na Real Madrid ili ajiunge Manchester City.

Jesus amekuwa na mwanzo mzuri England baada ya kutua Etihad kwa pauni milioni 27 katika usajili wa dirisha dogo la Januari akitokea Palmeiras ya Brazil.

Tayari amefunga mabao matatu kwenye Premier League ikiwa ni pamoja na yale mawili aliyofunga dhidi ya Swansea wikiendi iliyopita.

"Nilimwambia achague City, nilimwambia na akanielewa," anaeleza Fernandinho.

Nyota wa Brazil Jesus (kushoto) na Fernandinho wakifurahia ushindi wa Manchester City dhidi ya Swansea


USISAHAU KUBONYEZA SUBSCRIBE HAPO
LIKE PAGE YETU YA FACEBOOK Saluti5

Post a Comment

 
Top
Nicolaus Trac