FILAMU YA “TEARS OF EZINNE 2” KUTOKA NOLLYWOOD NI ZAIDI YA PICHA

FILAMU mpya iitwayo “Tears Of Ezinne 2” ni zaidi ya picha na ndio kwanza inaingia sokoni kutoka Nollywood lakini tayari imewaweka watu roho juu.

Wahusika wakuu ni watu wa familia ya Okagwe akiwemo Ezinne na dada zake kama akiwa Ada na mkubwa wao Ugonna.

Ukiitazama japo kwa harakaharaka utakiri kuwa inaweza kuwa miongoni mwa kazi bora zaidi kwa mwaka 2017 na hutasita kuipongeza familia ya Okagwe kwa kuandaa kazi nzuri.

Filamu hiyo imeandaliwa msituni katika mandhari ya kuvutia na wakati mwingine kutisha kupita maelezo, kwa wale wapenzi wa filamu sio kitu cha kukosa kabatini kwako.


Kinara wa filamu hii, Chinyere Ubah ambaye amezoeleka sana kwa ubora wa kazi zake.

No comments