GARETH BALE ATANGAZA KUONDOKA REAL MADRID

HAKUNA namna ya kueleza zaidi ya kusema winga ghari katika La Liga Gareth Bale ametangaza kuihama Real Madrid mara baada ya kumaliza kandarasi yake inayo malizika mwaka 2022.

Winga huyo wa zamani wa Totenam Hot Spurs ameweka bayana azma hiyo baada kuonekana hana haja ya kubaki kutumia katika La Liga hivyo anataka kubadilisha mazingira.

Hata hivyo imebainika kuwa hatua ya Bale kuondoka Madrid inatokana na kukwama kwa mpango wa kutaka aongezwe mshahara unaofanana na Cristiano Ronaldo.

Bale amekuwa akiuomba uongoza wa juu wa klabu hiyo kuwa anahitaji dau la mshahara unaofanana na Ronaldo sambamba na marupulupu mengine.

Lakini uongoza wa sasa chini ya kocha Zinedine Zidane na rais Florentino Perez imeshindwa kuketi mezani kwa ajili kujadili masilahi anayohitaji winga huyo na ndio inayomfanya Bale atangaze kuitimka pindi kandarasi yake ikifika tamati mwaka 2022.

Wote wawili wanatajwa katika uvumi wa kutaka kurejea katika Ligi ya premier huku wakihusishwa na kujiunga na kati ya Manchester United lakini huku waki mtengea kitita cha pauni mil 100.

No comments