Habari

GARETH BALE SASA KUBAKI SANA TU VIUNGANI SANTIAGO BERNABEU

on

SASA ni dhahiri kiungo wa Real Madrid, Gareth Bale hawezi kuondoka katika
miaka ya hivi karibuni ndani ya viunga vya Santiago Bernabeu.
Hii ni baada ya kuwepo kwa mazungumzo mapya ya kutaka awe mchezaji wa
kudumu licha ya kandarasi yake ya sasa kuonyesha inafikia tamati ifikapo mwaka
2022.
Winga huyo raia wa Wales sasa amejifunga pingu kwa miaka sita hadi mwishoni
mwa mwaka 2022, lakini kocha wake Zinedine Zidane ameomba Bale awe na mkataba
mrefu zaidi ikiwezekana hadi mwaka 2026.
Bale mwenye umri wa miaka 28, alitua Real Madrid mwaka 2013 akitokea
Tottenham Hotspur kwa dau lililovunja rekodi wakati ule, la pauni mil 86.

Taarifa za ndani ya klabu hiyo ya jijini Madrid zinabainisha kuwepo kwa
mazungumzo yanayoendelea hivi sasa ya kutaka kiungo huyo amalize maisha yake ya
soka ndani ya Madrid.

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *