"GHANA ILIPONZWA NA DHARAU KWA CAMEROON FAINALI ZA KOMBE LA MATAIFA YA AFRIKA"

INGAWA wapo wanaosema kuwa ni ajali, lakini wengi wanaamini Ghana “Black Stars” iliingia uwanjani kwa dharau dhidi ya Cameroon ndio maana wakachapwa mabao 2-0 katika nusu fainali ya Afrika.

Hiyo ni kutokana na rekodi ya mchezo wa nyuma, kabla ya mchezo wa nusu fainali timu hizo zilikutana mara 14, Ghana wakishinda mechi tano, Cameroon wakishinda mechi mbili na wakitoka sare mara sita.

Pengine rekodi hiyo ndiyo iliyowafanya Ghana kubweteka na matokeo wakajikuta wakilia kilio kisicho na faida tena.


Pengine Ghana walisahau kuwa matokeo waliyoyapata Cameroon katika robo fainali dhidi ya Senegal yaliwapa nguvu na kujiamini zaidi licha ya kuwa na kilio cha posho.

No comments