GIGGS ASEMA ZLATAN IBRAHIMOVIC NA ERIC CANTONA WANASHABIHIANA

NYOTA wa zamani wa Manchester United Ryan Giggs amesema kwamba kuna vitu vinavyoshabihiana kati ya staa mwenzake wa zamani Eric Cantona na straika wa sasa wa timu hiyo, Zlatan Ibrahiomovic.

Tangu awasilili katika klabu hiyo ya Old Trafford akiwa mchezaji huru Jurai mwaka huu, Ibrahimovic amekuwa moto wa kuotea mbali ambapo hadi sasa ameshazifumania nyavu mara i5 katika michezo 24 aliyocheza kwenye michuano ya Ligi Kuu England.

Kama ilivyo kwa straika huyo pia Cantona alifanya makubwa alipowasili Man United mwaka 1992 akitokea katika timu ya Leeds ambapo pia alisaidia timu hiyo kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ukiwa ni msimu wa kwanza kwa kocha Alex Ferguson.

“Nadhani kuna vitu wanavyofanana kwa sababu kila mmoja anajiamini na jinsi anavyoweza kufunga mabao”, alisema Giggs.


“Huwezi kuamini kwamba Eric ama Ibrahimovic wangeweza kuja Man United na kuwa wachezazji tegemeo,” aliongeza staa huyo wa Zamani.

No comments