GIGGS ASHAURI MAKOCHA WAZAWA WAPEWE NAFASI ENGLAND

STAA wa zamani wa Manchester United, Ryan Giggs amesema anaamini kuna wakufunzi na mameneja wengi kutoka nje, katika Ligi Kuu ya England na kwamba Waingereza hawapewi nafasi.

Winga huyo wa zamani wa Manchester United na Wales alisema idadi kubwa ya wakufunzi hao kutoka nje inawanyima wenyeji nafasi ya kujiendeleza.

Gigs, 43, alikuwa kaimu meneja kwa mechi nne United baada ya David Moyes kufutwa mwaka 2014 na baadae alifanyakazi kama msaidizi wa Louis Van Gaal.

“Sidhani kama kuna makocha Waingereza wa kutosha kwenye Ligi kwa sasa,” alisema.

“Ni vyema kuona mkufunzi Mwingereza akipewa nafasi. Nafikiri ni muhimu. Kuna wakufunzi wengi wazuri kutoka nje ya Ligi ya premier lakini pia kuna wakufunzi wengi na mameneja Waingereza huko nje.”

Kwa sasa ni klabu saba pekee kati ya 20 zinazocheza EPL ambazo zina mameneja Waingereza.

Gigs ambaye amesema hana haraka kurejea kazi ya ukufunzi, amesema ufanisi wa Paul Clement katika Swansea City ni ishara wakufunzi Waingereza wanaweza kufanikiwa.


Kwenye Ligi kwa sasa klabu saba zilizo juu kwenye jedwali zimo chini ya wakufunzi kutoka nje. Wa juu zaidi ambao wamo chini ya Mwingereza ni West Brom ambao wako chini ya Tony Pulis kutoka Wales.

No comments