GRIEZMANN ASHAURIWA KUJIPELEKA MANCHESTER UNITED ILI KUTENGENEZA JINA LA HESHIMA KAMA BECKHAM

HUU ni ushauri tu! Antoine Griezmann wa Atletico Madrid ameambiwa kama anataka kuliweka juu jina la heshima, anatakiwa ajiunge na Manchester United.

Kisha akaambiwa sababu ambayo inaweza ikampa akili mpya kwamba hata David Beckham anayemhusudu alipata mafanikio akiwa na United kabla ya kujiunga na klabu nyingine.

Ushauri huo umetoka kwa mshauri wa mwanasoka huyo, Sebastien Bellencontre ambaye ameajiriwa na Griezmann kwa ajili ya kumshauri katika masuala muhimu ya kumjenga katika maisha ya kisoka.

Katika ushauri huo, Bellencontre alimwambia mteja wake huyo aachane na ndoto za kutaka kujiunga na klabu nyingine zinazomuhitaji ili afikirie zaidi kutua Old Trafford kwa ajili ya mafanikio ya baadae.

Hatua ya mshauri huyo inakuja katika ukweli kuwa Griezmann amekuwa na ndoto za kufikia mafanikio ya David Bekham na amekuwa akimuhusudu kiungo huyo wa zamani wa klabu za Manchester United na Real Madrid.

Pamoja na ushauri huo, klabu za barcelona, Bayern Munich na Real Madrid zimekuwa katika mbio za kumwania ifikapo usajili wa majira ya kiangazi mwaka huu.

Hata hivyo, klabu ya Manchester United wamekuwa mstari wa mbele kusaka saini ya straika huyo ambaye amekuwa katika kiwango kizuri tangu katika mashindano ya Klabu Bingwa Ulaya yaliyofanyika nchini Ufaransa mwaka jana.

United chini ya kocha Jose Mourinho wameweka mezani ofa nono ya pauni mil 85 kwa ajili ya Griezmann na tayari uongozi wa juu wa mashetani hao ushatia baraka za uamui huo.


“Nimesikia ya Griezmann kutakiwa na klabu mbalimbali kubwa, lakini nimemweleza atulize akili kwa ajili ya kutimiza ndoto za kufuata nyayo za David Bekham,” alisema Bellencontre akihojiwa na magazeti ya michezo nchini Ufaransa.

No comments