GUARDIOLA AMPIGIA HESABU KALI GAMEIRO USAJILI WA KIANGAZI

STRAIKA wa Atletico Madrid, Kevin Gameiro ameingia katika rada za kocha Pep Guardiola kwa ajili ya usajili wa majira ya kiangazi.

Gameiro mwenye umri wa miaka 29, mzaliwa wa Ufaransa yupo katika kiwango cha juu tangu kuanza kwa msimu huu, hali hiyo ndio inawafanya Man City waingie katika mazungumzo ambayo yanasimamiwa na kocha Guardiola.

Pep amenukuliwa na Sky Sports juu ya azma ya kumnasa mpachika mabao huyo muhimu wa klabu ya Sevilla ya Hispania na kwamba mazungumzo yanakwenda vizuri.

Akinukuliwa, kocha Pep Guardiola alisema: “Nina orodha ya wachezaji wengi mezani kwangu, lakini kati ya hao ni huyu Gameiro. Ni mchezaji wa kiwango na anatambua majukumu.”

“Nimeingia mbioni kwa ajili ya kumsajili na nitahakikisha ninafanikisha hili,” alisisitiza Guardiola.


“Mkakati wangu wa sasa ni kuimarisha kikosi, tuna majina mengi ya kuyafuatilia wakati huu, lakini nitaanza na Gameiro na kisha nitaangalia nani mwingine kwa ajili ya kuifanya City iwe ya mafanikio na ushindi,” ameongeza Pep.

No comments