Habari

HATIMAYE SIKU IMEWADIA, USIKU WA ISHA MASHAUZI HAPATOSHI MANGO GARDEN LEO USIKU …jikumbushe na picha 12 za show ya mwaka jana

on

Usiku wa Isha Mashauzi (Isha’s Night) unaosindikizwa na burudani ya
nguvu kutoka kwa kundi zima la Mashauzi Classic, unafanyika leo usiku ndani ya
ukumbi wa Mango Garden Kinondoni.
Tayari onyesho hilo limekuwa gumzo kubwa na Mango Garden inategewa
kulipuka kwa shangwe za kila aina.
Ni onyesho linalofanyika kila mwaka na huambatana na wiki ya kuzaliwa
(Birthday) ya Isha Mashauzi ambapo mwanamama huyo huitumia siku yake hiyo
maalum kumimina burudani ya ‘level’ nyingine.
Isha Mashauzi ameiambia Saluti5 kuwa atakuwa na ratiba safi
itakayoufanya usiku huo uwe wa kipekee, lakini yote kwa yote yale masaa yake
mawili ya kumimina burudani mfululizo yatakuwepo kama ilivyo ada ya ‘Isha’s
Night’.
“Nitaimba nyimbo zisizopungua saba, lakini pia tutakata keki kwa Team
February wote, kutakuwa na shampeni bila kusahau red carpet kwaajili ya picha
za mnato,” alisema Isha Mashauzi.

JIKUMBUSHE KIDOGO ILIVYOKUWA KWENYE SHOW YAKE YA MWAKA JANA
 Isha Mashauzi akizungumza machache kwenye birthday yake ya mwaka jana
 Isha Mashauzi akimlisha keki mpiga solo wa Jahazi, Emeraa katika Isha’s Night ya mwaka jana
 Isha Mashauzi akiimba kwa hisia mwaka jana mwezi kama huu
Baadhi ya keki za birthday ya Isha Mashauzi za mwaka 2016
Wadau MC Double A (kushoto) na Shakoor Jongo nao walikuwepo kwenye Isha’s Night ya mwaka jana
 Isha Mashauzi akiimba mbele ya mashabiki wake Isha’s Night ya mwaka jana
Makamuzi kwa kwenda mbele
Waimbaji wa Mashauzi Classic Saida Mashauzi (kushoto) na Naima Mohamed waki-show love katika Usiku wa Isha Mashauzi 2016
Wadau wanaojiita Team Mashauzi wakifanya yao ukumbini kwenye Isha’s Night ya mwaka jana
Team Mashauzi katika picha ya pamoja katika Isha’s Night ya mwaka jana
Mango Garden palivyopendeza Isha’s Night ya mwaka jana

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *