HENRIKH MKHITARYAN AMWOMBA MUNGU KUHUSU MAJERAHA YAKE

LICHA ya kuifungia bao la ushindi timu yake ya Manchester United dhidi ya Saint – Etiene katika michuano ya Ligi ya Europe, staa Henrikh Mkhitaryan amesema kuwa bado anamuomba Mwenyezi Mungu kumnusuru na majeraha yanayomkabili.

Baada ya kuifungia Man United bao lake la nne katika dakika ya 16 ya mchezo huo wa pili uliopigwa katika uwanja wa Stade Geoffroy - Guichard, nafasi ya Mkhitaryan iliyochukuliwa na Marcus Rashford zikiwa ni dakika tisa baada ya kupachika bao hilo baada ya kukumbwa na majeraha ya misuli ya nyama za paja.

Hata hivyo, pamoja na kukumbwa na hali hiyo baadae alituma ujumbe kupitia mtandao wake wa kijamii wa Twitter akielezea jinsi alivyojisikia furaha kwa kuweza kupachika bao hilo akiwa nchini Ufaransa ambako alikulia.

Katika ujumbe huo, staa huyo mwenye umri wa miaka 28 alielezea pia kusikitishwa kwake kwa kuikosa safari ya kwenda katika uwanja wa Wembley ambako Man United itaivaa Southampton katika mchezo wa Kombe la Ligi, lakini akasema kuwa bado anamuomba Mungu aweze kumponya kwa haraka.


“Nashukuru nimeweza kufunga bao lakini namuomba Mwenyezi Mungu aweze kuniponya kwa haraka,” alisema staa huyo kupitia ujumbe huo.

No comments