HUSSEIN JUMBE ANADI NYIMBO MBILI MPYA TALENT BAND... aomba mashabiki kuzipiokea

BOSI wa Talenti Band, Hussein Jumbe amewaomba mashabiki wake kuzipokea nyimbo zao mbili mpya.

Akiongea na saluti5, Jumbe ambaye ni kati ya watunzi mahiri Bongo, alisema kwamba nyimbo hizo ni maandalizi ya albamu ya kwanza ya Talent Band kwa mwaka huu, 2017.


“Baada ya hivi karibuni kuzindua albamu ya “Kipima Joto”, Talent Band inakuja na nyimbo mbili mpya ambazo ni “Wasiwasi wa Nini” iliyotungwa na Fadhili Musafi na “Ukisema Cha Nini” ya Asia yahya,” amesema Jumbe.

No comments