ISCO AMLETEA POZI KOCHA ZIDANE KUONGEZA MKATABA REAL MADRID

NYOTA wa Real Madrid, Francisco Romain Alarcon Suarez maarufu kama “Isco” anakaribia kumaliza mkataba wake katika klabu hiyo na hakuna dalili kwamba anataka kubaki klabuni hapo.

Gazeti la Marca limeandika kwamba mchezaji huyo ameongea mara mbili na kocha Zinedine Zidane kuhusu uwezekano wa kuongeza mkataba lakini mazungumzo hayo ni kama yamegonga mwamba.


Badala yake imedaiwa kwamba mchezaji huyo anafikiria kuhamia ama Juventus ya Italia au Manchester City ya Uingereza kwa ajili ya kubadili upepo.

No comments