ISHA MASHAUZI AINGIA STUDIO KUPAKUA “MWANAMKE MPANGO MZIMA” … ni zawadi maalum kwa wanawake


Mwimbaji bora wa kike wa taarab Isha Mashauzi ameingia studio kupika wimbo mpya maalum kwaajili ya wanawake.

Wimbo unakwenda kwa jina la “Mwanamke Mpango Mzima” ambao umepigwa kwenye miondoko ya chakacha lakini ndani yake kukiwa na vionjo vya dansi na taarab.

“Mwanamke Mpango Mzima” ambayo ina urefu wa dakika 3 na sekunde 55 inapikwa katika studio za Soft Records chini ya producer Pitchou Mechant.

Isha Mashauzi ameiambia Saluti5 kuwa ngoma hiyo ni zawadi maalum kwa wanawake wenzake na anatarajia kuiachia rasmi mwishoni mwa mwezi huu ili isindikize Siku ya Wanawake Duniani ambayo hufanyika Machi, 8 kila mwaka.

“Ni wimmbo mzuri, una ujumbe mzuri, unachezeka na unaweza kutumika kwenye kampeni zozote za harakati za kumtetea mwanamke, lakini pia unaweza kufaa kwenye sherehe mbali mbali kama send off na kitchen party,” anafafanua Isha.

"Mwanamke Mpango Mzima" ni moja ya project binafsi za Isha Mashauzi nje ya bendi yake ya Mashauzi Classic.

No comments