ISHA MASHAUZI KURINDIMA KAHAMA VALENTINE'S DAY


Mwimbaji bora wa kike wa taarab Isha Mashauzi, atakuwa Kahama mjini siku ya wapendanao duniani (Valentine's Day).

Isha atangurumisha burudani zake katika ukumbi wa Kikwetu Kwetu ulioko maeneo ya Nyahanga.

Mwimbaji huyo anayetesa pia katika miondoko ya rumba, ameiambia Saluti5 kuwa onyesho hilo litafanyika Jumanne ya tarehe 14 mwezi huu na kwamba moja ya zawadi anayokwenda nayo Kahama ni wimbo wake wa Kismet ambao kwasasa unatamba sana katika audio na video.

“Watu wa Kahama wategemee burudani ya nguvu kutoka kwangu, kuanzia taarab hadi rumba,” alisema Isha.

No comments