JAHAZI MODERN TAARAB ‘WAREJEA’ TRAVERTINE HOTEL


Kundi la Jahazi Modern Taarab litarejea kwenye ukumbi wake wa zamani wa nyumbani Travertine Hotel, Magomeni jijini Dar es Salaam kwa onyesho maalum la Valentine’s Day.

Jahazi ilikuwa ikipatikana Travertine Hotel kila Jumapili kabla haijandoka ukumbini hapo mwezi Novemba mwaka jana.

Mmoja wa mabosi wa Jahazi, Hamis Boha, ameiambia Saluti5 kuwa Jumanne ijayo, kundi hilo litajitosa Travertine na kuangusha burudani ya nguvu kwaajili ya Siku ya Wapendanao inayofanyika kila tarehe 14 Februari.

Boha amesema hiyo itakuwa fursa kwa mashabiki wao kuzishuhudia ‘live’ nyimbo mpya kabisa za Jahazi sambamba na wasanii wapya.


No comments