Habari

JAMIE CARRAGHER AMMIMINIA SIFA HENRIKH MKHITARYAN… awapond Ozil, Silva, Mata

on

MCHAMBUZI wa
michezo katika runinga ambaye ni nyota wa zamani wa klabu ya Liverpool, Jamie Carragher amesema uwezo wa mchezaji Henrikh Mkhitaryan uko juu kwa sasa.
Mkongwe huyo
amesema kwamba uwezo wa kiungo huyo umewafunika kabisa nyota wengine
wanaotakata katika Ligi Kuu ya Uingereza wakiwamo Ozil, Silva na Mata.
Akizungumzia
kuhusu uwezo wa nyota huyo wa Manchester United ambao ameuonyesha kwenye mechi dhidi
ya Leicester City, Jamie alisema Mkhitaryan ana kitu ambacho ni wachezaji wachache sana walionacho.
Kwa mujibu
wa nyota huyo, kitu chenyewe ni uwezo wa kuwa na kasi inayofanana na kwa muda
wote.
Amesema
wachezaji kama Mesut Mustafa Ozil wa Arsenal, Juan Manuer Mata Garcia wa Man United, David Josue Jimenez Silva wa Man City, ni watu ambao wana uwezo mkubwa sana
kwenye kutoa pasi lakini Mkhitaryan yupo kwenye kiwango kingine kabisa.

Mkhitaryan amekuwa
chaguo kubwa kwenye kikosi chake na uwezo wake mkubwa umekuwa ukiwafurahisha
washabiki wengi kutokana na kasi na aina ya pasi anazotoa.

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *