JAVIER PASTORE AFICHUA KUWA KATIKA RADA ZA KOCHA ANTONIO CONTE

NYOTA wa klabu ya PSG Javier Pastore amekiri kuwindwa na kocha wa sasa wa Chelsea, Antonio Conte ingawa mpango huo umeshindwa kukamilika katika usajili wa mwezi Januari ambalo dirisha lake limefungwa Jumanne iliyopita.

Kocha Conte alimweka katika orodha yake ya wachezaji anaowawania.

Akinukuliwa Pastore amesema ndoto za Conte ziliyeyuka baada ya PSG kukataa ofa ya kuuzwa kwake.

“Bado nipo PSG najisikia furaha kuwa hapa hakuna tatizo kuwa hapa.”

“kucheza timu inayoshiriki Ligi ya Mabingwa ni klati ya malengo yangu pia kila mchezaji anaota mafanikio kama hayo.”

“Ninatarajiwa kuwa katika kiwango hicho cha mafanikio ninaamini kuna siku nitafikia hatua hiyo, ni suala la kusubiri kuona” alisisitiza Pastore.

No comments